Leviticus 24

Mafuta Na Mikate Mbele Za Bwana

1 Bwana akamwambia Musa, 2 a“Waagize Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili taa ziwe zinawaka daima. 3 bNje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Haruni ataziwasha taa mbele za Bwana kuanzia jioni hadi asubuhi bila kuzima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. 4 cTaa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele za Bwana lazima zihudumiwe daima.

5 d“Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efa
Sehemu mbili za kumi za efa ni sawa na kilo mbili.
za unga kwa kila mkate.
6 fIweke katika mistari miwili, kila mstari mikate sita, uiweke mbele za Bwana juu ya meza iliyotengenezwa kwa dhahabu safi. 7 gKando ya kila mstari, weka uvumba safi kama sehemu ya kumbukumbu ili kuwakilisha mikate kuwa sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa kuteketezwa kwa moto. 8 hMikate hii itawekwa mbele za Bwana kila wakati, Sabato baada ya Sabato, kwa niaba ya Waisraeli, kuwa Agano la kudumu. 9 iHii ni mali ya Haruni na wanawe, watakaoila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni sehemu takatifu sana ya fungu lao la kawaida la sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa kuteketezwa kwa moto.”

Mwenye Kukufuru Apigwa Mawe

10Basi mwana wa mama Mwisraeli na baba Mmisri alikwenda miongoni mwa Waisraeli, nayo mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli. 11 jHuyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru Jina la Bwana kwa kulaani; kwa hiyo wakamleta kwa Musa. (Jina la mama yake aliitwa Shelomithi binti wa Dibri, wa kabila la Dani.) 12 kNao wakamweka mahabusu mpaka mapenzi ya Bwana yawe wazi kwao.

13Ndipo Bwana akamwambia Musa: 14 l“Mchukue huyo aliyekufuru nje ya kambi. Wale wote waliomsikia akikufuru wataweka mikono juu ya kichwa chake, kisha kusanyiko lote litampiga mawe. 15 mWaambie Waisraeli: ‘Ikiwa mtu yeyote atamlaani Mungu wake, atakuwa na hatia kwa uovu wake; 16 nyeyote atakayekufuru Jina la Bwana ni lazima auawe. Kusanyiko lote litampiga kwa mawe. Iwe ni mgeni au mzawa, atakapolikufuru Jina la Bwana, ni lazima auawe.

17 o“ ‘Kama mtu yeyote atamuua mtu mwingine, ni lazima auawe. 18Mtu yeyote auaye mnyama wa mtu mwingine lazima afidie, uhai kwa uhai. 19Ikiwa mtu yeyote atamjeruhi jirani yake, chochote alichomtenda naye atatendewa: 20 piwapo amemvunja mfupa atavunjwa mfupa, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama alivyomjeruhi mwenzake, vivyo hivyo ndivyo atakavyojeruhiwa. 21 qYeyote auaye mnyama wa mtu lazima alipe fidia, lakini yeyote auaye mtu, lazima auawe. 22 rMtakuwa na sheria iyo hiyo kwa mgeni na kwa mzawa. Mimi ndimi Bwana Mwenyezi Mungu wenu.’ ”

23 sKisha Musa akasema na Waisraeli, nao wakamchukua yule aliyekufuru nje ya kambi na kumpiga mawe. Waisraeli wakafanya kama Bwana alivyomwagiza Musa.
Copyright information for SwhKC